CHINA-UCHUMI

China yapokea kwa mikono miwili mazungumzo ya kibiashara na Marekani

Bendera za China na Marekani zinapepea nje ya jengo la kampuni moja huko Shanghai, China Aprili 14, 2021.
Bendera za China na Marekani zinapepea nje ya jengo la kampuni moja huko Shanghai, China Aprili 14, 2021. © REUTERS/Aly Song//File Photo

China imekaribisha kuanza tena kwa "mazungumzo ya kawaida" na Marekani juu ya maswala ya biashara na uchumi, ikihakikisha kwamba pande hizo mbili sasa zinataka kumaliza tofauti zao kwa njia ya busara.

Matangazo ya kibiashara

Naibu wa Waziri Mkuu wa China Liu He, ambaye anaongoza mazungumzo kwa niaba ya Beijing, alikutana mara mbili kwa wiki moja katika mkutano kwa njia ya video na mwakilishi wa Biashara wa Marekani Katherine Tai na Katibu katika wizara ya fedha Janet Yellen.

Mazungumzo haya yalikuwa mawasiliano ya kwanza rasmi kati ya nchi hizo mbili juu ya suala hili tangu Rais wa Marekani Joe Biden alipochukuwa hatamu ya uongozi wa nchi mwezi wa Januari mwaka huu.

Kuanza tena kwa mazungumzo kati ya China na Marekani kunakuja baada ya mvutano mkali chini ya utawala wa Rais wa zamani Donald Trump.

Katika taarifa yake, Washington, kwa upande wake, imesisitiza juu mazunumzo ya kweli na China. Janet Yellen na Katherine Tai wamesema wanatarajia mazungumzo zaidi na Liu He.