MAREKANI-CHINA

Biden ayaweka orodha nyeusi makampuni 59 ya ulinzi na teknolojia ya China

Rais wa Marekani Joe Biden.
Rais wa Marekani Joe Biden. REUTERS - CARLOS BARRIA

Rais wa Marekani Joe Biden siku ya Alhamisi alisaini agizo jipya linalokataza mashirika ya Marekani kuwekeza katika kampuni karibu 60 za China na zenye uhusiano na sekta ya ulinzi na teknolojia ya uchunguzi.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na utawala wake, mpango huu unapanua wigo wa maandishi ya zamani kutoka kwa urais Donald Trump, ambayo yalionyesha makosa ya kisheria.

Wizara ya Fedha ya Marekani itatekeleza na kusasisha orodha hii nyeusi "kila wakati", maafisa wakuu wa utawala wasema. Orodha hii - inayojumuisha kampuni 59 za China ambazo mashirika ya Marekani yatakatazwa kununua au kuuza hisa - itachukua nafasi ya orodha ya sasa ya wizara ya Ulinzi na itaanza kutumika Agosti 2, wamesema.

Lengo ni kuzuia msaada na uwekezaji wa Marekani katika viwanda vya kijeshi vya China, lakini pia ujasusi wa kijeshi na pia mipango ya utafiti na maendeleo katika sekta ya usalama, amesema Joe Biden katika agizo hilo.