BELARUS-VIKWAZO

EU kupiga marufuku mashirika ya ndege ya Belarus kupitia kwenye anga yake

Ndege aina ya Boeing 737-800 ya shirika la ndege la Belarus la Belavia inaondoka katika Uwanja wa ndege wa Domodedovo nje ya Moscow, Urusi Mei 28, 2021.
Ndege aina ya Boeing 737-800 ya shirika la ndege la Belarus la Belavia inaondoka katika Uwanja wa ndege wa Domodedovo nje ya Moscow, Urusi Mei 28, 2021. REUTERS - MAXIM SHEMETOV

Mabalozi wa nchi za Umoja wa Ulaya leo Ijumaa walmeidhinisha mpango wa kupiga marufuku ndee za mashirika ya ndege ya Belarus kutua katika viwanja vya ndege katika nchi zilizo katika umoja huo, au hata kuruka juu ya anga zao, wanadiplomasia watatu wamesema.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ni sehemu ya vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Belarus, ambayo Mei 23, ililazimisha ndege ya shirika la ndege la Ryanair iliyokuwa imembeba mpinzani wa rais wa Belarus kutua Minsk chini ya aizo la Rais Alexander Lukashenko,

Bila pingamizi la dakika ya mwisho kutoka kwa nchi wanachama, hatua hii lazima ianze kutekelezwa kutoka saa sita usiku saa za Ulaya ya Kati (CET), wameongeza wanadiplomasia hawo.

Umoja wa Ulaya pia unapendekeza, bila hata hivyo kuyapia marufuku, mashirika ya ndege kutoka kambi hiyo kuepuka kuruka juu ya anga ya Belarus.Kulingana na Eurocontrol, mamlaka ya Ulaya ya ukaguzi wa safari za ndege, karibu ndege 400 za raia huruka juu ya anga ya umoja huo kila siku.

Lufthansa, SAS, Air France, LOT, Finnair na airBaltic ni miongoni mwa mashirika ya ndege ambayo tayari yametangaza kuwa hayataruka tena juu ya anga ya Belarus.

Kiongozi wa upinzani nchini Belarus Svyatlana Tsikhanouskaya pia ametoa wito kwa Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulaya kushirikiana ili kutoa shinikizo zaidi kwa Alexander Lukashenko.

Sviatlana Tsikhanouskaya, ambaye alikuwa akizungumza wakati wa ziara yake huko Warsaw kabla ya mkutano wa kilele wa G7 uliopangwa kufanyika Juni 11-13, alisema ana matumaini kuwa maswala yaliyowasilishwa na upinzani wa Belarus yatashughulikiwa wakati huu.