HONG KONG-HAKI

Beijing yazishtumu balozi za Marekani na EU kuwasha mishumaa ya Tiananmen

Mishumaa ikiwaka kwenye madirisha ya ubalozi wa Marekani huko Hong Kong, Juni 4, 2021.
Mishumaa ikiwaka kwenye madirisha ya ubalozi wa Marekani huko Hong Kong, Juni 4, 2021. © AFP - PETER PARKS

Mamlaka nchini China imebaini kwamba mishumaa iliyowashwa na balozi za Marekani na Umoja wa Ulaya huko Hong Kong kuadhimisha matukio ya Juni 4, 1989 huko Tiananmen ni "tamasha la kisiasa lisilofaa" lililolenga kuhatarisha usalama wa eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mwaka wa pili mfululizo, sherehe ya kuwakumbuka waathiriwa wa ukandamizaji wa Tiananmen mwka wa 1989 imepigwa marufuku hkatika jimbo la Hong Kong: mikusanyiko imepigwa marufuku, lakini pia kuzungumzia juu ya matukio haya au kuyafananisha au kuyataja kumepiwa marufuku.

Mishumaa iliwashwa Ijumaa jioni kwenye madirisha ya jengo la ubalozi wa Marekani, ambalo lio karibu na makazi ya kiongozi wa Hong Kong aliyeteuliwa na Beijing, Carrie Lam, na vile vile ofisi ya Umoja wa Ulaya.

Maadhimisho yaliyopiwa marufuku

Mpango ambao haukufurahisha Beijing. "Jaribio lolote la kuitumia Hong Kong kukaidi au kufanya shughuli zozote zilizo kinyume na mamlaka katika eneo hilo linavuka mstari mwekundu (...), ni jambo ambalo halivumiliki kabisa," amesema msemaji wa ofisi ya Hong Kong ya Wizara ya Mambo ya nje ya China.

"Tunasisitiza tena vyombo vya nchi zinazohusika huko Hong Kong kukoma (...) kuingilia masuala ya Hong Kong na mambo ya ndani ya China kwa jumla, na kuepuka kucheza na moto," ameongeza. Mikusanyiko n maandamano yliyofanyika Juni 4 yanaonekana kama ishara ya matarajio ya kidemokrasia ya Hong Kong.

Hata hivyo kwa miongo mitatu huko Hong Kong, umati mkubwa wa watu walikesha, huku wakiwasha mishumaa Juni 4 ikiwa ni kumbukumbu ya wale waliouawa mnamo mwaka 1989 wakati wa ukandamizaji wa vuguvugu la demokrasia huko Beijing.