CHINA

China: Wawili wafariki dunia, sita watoweka katika mgodi wa makaa ya mawe

Mgodi wa Makaa ya mawe wa Xinhua katika Mkoa wa Henan, China.
Mgodi wa Makaa ya mawe wa Xinhua katika Mkoa wa Henan, China. Reuters

Ajali katika mgodi wa makaa ya mawe katikati mwa China imesababisha watu wawili kupoteza maisha na wengine sita bado hawajapatikana, kituo cha serikali cha CCTV kimeripoti leo Jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

"Mlipuko wa bahati mbaya" ulitokea kwenye mgodi wa makaa ya mawe unaosimamiwa na kampuni ya Henan Hebi Coal and Electricity Co Ijumaa jioni na mamlaka katika mkoa wa Henan umetangaza mpango wa dharura, kituo cha CCTV kimeongeza.

China imezindua ukaguzi wa usalama katika migodi yake ya makaa ya mawe kote nchini, lakini bei rekodi za madini zimesababisha makampuni ya uchimbaji madini kuongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya ulimwengu.

Mwezi Mei mwaka huu Beijing pia iliahidi kufanyia kazi suala la kuweka sawa bei za malighafi, huku ikihimiza wazalishaji wake wa makaa ya mawe kujitokeza kwa wingi.