MYANMAR-USALAMA

Myanmar: Mapigano yaenea katika Delta ya Irrawaddy, watu kadhaa wauawa

Watu waliolazimika kuyahama makazi yao kufuati mapigano kaskazini-magharibi mwa Myanmar kati ya vikosi vya jeshi na wapiganaji wanaopinga utawala wa kijeshi katika Jimbo la Chin, Myanmar, Mei 31, 2021.
Watu waliolazimika kuyahama makazi yao kufuati mapigano kaskazini-magharibi mwa Myanmar kati ya vikosi vya jeshi na wapiganaji wanaopinga utawala wa kijeshi katika Jimbo la Chin, Myanmar, Mei 31, 2021. REUTERS - STRINGER

Watu wasiopungua watatu wameuawa katika Bonde la Irrawaddy nchini Myanmar katika makabiliano kati ya wanajeshi na wanakijiji, vyombo vya habari na wakaazi wameripoti, wakati mapigano pia yameripotiwa Kaskazini na Mashariki mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi limejitahidi kwa miezi minne kuweka udhibiti wake tangu liliporudi madarakani katika katika mapinduzi ya Februari 1. Mapinduzi hayo yalimwondoa kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia Aug San Suu Kyi baada ya muongo mmoja wa mageuzi ya kidemokrasia ambayo yalifungua nchi hii iliyotengwa ya Kusini Mashariki mwa Asia.

Maandamano dhidi ya jeshi linaloshikilia madaraka nchini Myanmar yanafanyika kila siku katika maeneo mengi ya nchi, pia yaliyozorota na migomo, wakati mivutano na makabila yenye silaha yanayopinga jeshi yameongezeka.

Mapigano yameripotiwa Jumamosi katika eneo la kilimo la Irrawaddy, eneo muhimu kwa uzalishaji wake wa mpunga. Kulingana na mkazi mmoja, makabiliano hayo yalianza kabla ya alfajiri huko Kyonpyaw, kilomita 150 kaskazini magharibi mwa Yangon, wakati wanajeshi walipokuja kumkamata mtu mmoja anayeshukiwa kusafirisha silaha na walikaribishwa kwa mlipuko wa bomu.

Kulingana na shirika la habari la REUTERS, shirika hilo halikuweza kumpata msemaji wa jeshi ili kuelezea juu ya makabiliano hayo au mapigano mengine yanayoripotiwa nchini Myanmar.

Tangu mapinduzi ya kijeshi, watu wasiopungua 845 wameuawa na vikosi vya usalama na zaidi ya 4,500 wamefungwa, kulingana na dtakwimu za wanaharakati. Wanajeshi waliopo madarakani wanafutilia mbali na takwimu hizi.