INDIA-BIASHARA

Mchele wa Basmati wazua tena mzozo kati ya India na Pakistan

Ombi la India limesababisha wimbi la hofu nchini Pakistan, ambayo ina hatari ya kupoteza soko muhimu la kuuza bidhaa hiyo nje ya nchi, na limechochea uhasama wa kihistoria kati ya nchi mbili zenye nguvu ya nyuklia zilizoanzishwa baada ya kugawanywa mwaka 1947.
Ombi la India limesababisha wimbi la hofu nchini Pakistan, ambayo ina hatari ya kupoteza soko muhimu la kuuza bidhaa hiyo nje ya nchi, na limechochea uhasama wa kihistoria kati ya nchi mbili zenye nguvu ya nyuklia zilizoanzishwa baada ya kugawanywa mwaka 1947. Arif ALI AFP

Kwa miezi kadhaa, India na Pakistan zimekuwa zikishtumiana kuhusu bidhaa ya mchele wa basmati, ambo ni kutoka nchi hizi mbili, ili kujua ni yupi atakayeruhusiwa kuuza chini ya jina hili katika Umoja wa Ulaya, mchele huu unathaminiwa sana na watumiaji.

Matangazo ya kibiashara

India imewasilisha kwa na Tume ya Ulaya ombi linalolindwa la Kijiografia (PGI) ambalo, ikiwa litakubaliwa, itaihakikishia matumizi ya kipekee ya jina la Basmati katika Umoja wa Ulaya.

Pakistan, nchi nyingine ambayo inayouza nje mchele huu wenye kunukia wenye punje ndefu na nzuri unaolimwa bondeni karibu na mlima wa Himalaya, imepinga mara moja ombi lililochapishwa mwezi wa Septemba 2020 katika Jarida Rasmi la Umoja wa Ulaya.

Ombi la India limesababisha wimbi la hofu nchini Pakistan, ambayo ina hatari ya kupoteza soko muhimu la kuuza bidhaa hiyo nje ya nchi, na limechochea uhasama wa kihistoria kati ya nchi mbili zenye nguvu ya nyuklia zilizoanzishwa baada ya kugawanywa mwaka 1947