MYANMAR-USALAMA

Ajali ya ndege ya jeshi la Myanmar yaua watu 12

Chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika. Myanmar ina historia ndefu ya ajali za ndege.
Chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika. Myanmar ina historia ndefu ya ajali za ndege. AP - Gemunu Amarasinghe

Watu 12 wamefariki dunia katika ajali ya ndege ya vikosi vya jeshi vya Myanmar iliyotokea leo Alhamis karibu na mji wa Mandalay, mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, idara ya huduma za dharura imesema.

Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo ilikuwa kwenye ilikuwa ikisafiri kati ya mji mkuu Naypyidaw na mji wa Pyin Oo Lwin wakati ilianguka karibu mita 300 kutoka kiwanda cha chuma, imeripoti televisheni ya Myawaddy, inayodhibitiwa na jeshi linaloshikilia madarakani tangu mapinduzi ya Februari 1.

Ndege hiyo ilikuwa imebeba wanajeshi sita na watawa kadhaa ambao wangelishiriki katika hafla katika kanisa ya Wabudhi, vyombo vingine vya habari vimeripoti.

Rubani na abiria mmoja wamenusurika na wamelazwa hospitalini, kulingana na shahidi.

Chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika. Myanmar ina historia ndefu ya ajali za ndege.