INDIA-USALAMA

India: Kumi na moja wafariki dunia, baada ya jengo kuporomoka

Waokoaji wanafuta manusura chini ya vifusi vya jengo lililoporomoka, Mumbai, India mnamo Juni 10, 2021.
Waokoaji wanafuta manusura chini ya vifusi vya jengo lililoporomoka, Mumbai, India mnamo Juni 10, 2021. REUTERS - HEMANSHI KAMANI

Takriban watu 11, ikiwa ni pamoja na watoto wanane, wamefariki duniaa baada ya jengo la makazi huko Bombay kuanguka Jumatano jioni, viongozi wa eneo hilo wamesema.

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo limetokea karibu usiku wa manane katika kitongoji cha Mumbai, viongozi wamebaini, wakiongeza kuwa watu zaidi wanaweza kuwa wamekwama chini ya vifusi.

Watu wanane wamejeruhiwa na kupelekwa katika hospitali za karibu, viongozi wamesema.

Visa vya kuporomoka kwa majengo hutokea mara kwa mara katika mji mkuu wa kiuchumi wa India, Bombay, wakati wa mvua ya masika.