MYANMAR-HAKI

Myanmar: Aung San Suu Kyi ashtakiwa kwa rushwa katika kesi ya tatu

Kiongozi wa zamani wa Myanmar Aung San Suu Kyi, akabiliwa na mashitaka matatu, ikiwa ni pamoja na ufisadi.
Kiongozi wa zamani wa Myanmar Aung San Suu Kyi, akabiliwa na mashitaka matatu, ikiwa ni pamoja na ufisadi. AP - Peter Dejong

Kiongozi wa zamani wa Myanmar Aung San Suu Kyi, aliyetimuliwa mamlakani kupitia mapinduzi ya kijeshi Februari 1, ameshtakiwa kwa ufisadi, gazeti la serikali la Global New Light of Myanmar limeripoti leo Alhamisi (Juni 10).

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa zamani wa serikali ya kiraia anashtumiwa hasa kwa kupokea "dola 600,000 na kilo kadhaa za dhahabu" kama hongo. Pia anashtakiwa kwa matumizi mabaya ya ardhi kwa shirika la kihisani la Daw Khin Kyi, ambalo alikuwa akiongoza.

Aung San Suu Kyi atatakiwa kujibu mashtaka yasiyopungua manne: kuhisiana na uchapishaji wa taarifa ambazo zinatajwa na jeshi kwamba huenda zinaweza kusababisha hofu au wasiwasi nchini humo.

Aung San Suu Kyi anatuhumiwa kukiuka sheria za mawasiliano pamoja na kunuia kuchochea vurugu zinazofanywa na uma wa Myanamar.

Awali wakili wake Khin Maung Zaw alisema kwamba hawana uhakika ni kesi ngapi nyingine zitamkabili mteja wao katika kipindi hiki kwa sababu wanamini hakuna kisichowezekana nchini humo.

Maandamano ya kupinga utawala wa kijeshi bado yanaendelea Myanmar

Alikamatwa mjini Naypyitaw, mji ulioko nje kabisa uliojengwa na jeshi na kuufanya ndio makao makuu yake wakati wa utawala wa kidikteta uliowahi kuwepo nchini humo.

Hata hivyo bado maandamano yanaendelea kushuhudiwa katika nchi hiyo ambapo, huku idadi ya vifo ikiendelea kuongezeka siku baada ya siku. Karibu watu 860 wameuawa nchini Myanmar.