JAPAN-MICHEZO

Michezo ya Olimpiki: Hofu yatanda Tokyo baada ya kuripotiwa visa vya maambukizi

Wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Tokyo Julai 15, 2021 wanaojiandaa kuwapokea wajumbe wa Michezo ya Olimpiki.
Wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Tokyo Julai 15, 2021 wanaojiandaa kuwapokea wajumbe wa Michezo ya Olimpiki. Kazuhiro NOGI AFP

Kuelekea michezo ya Olimpiki jijini Tokyo nchini Japan, Ijumaa, wiki hii, mmoja wa waandalizi wa michezo hiyo ameambukizwa virusi vya Corona, akiwa kwenye kijiji walichofikia wachezaji mbalimbali.

Matangazo ya kibiashara

Mpaka sasa kuna visa 15 vya maambukizi ya Corona ambavyo vimeripotiwa kuhusiana na maandalizi ya michezo hii na inamaanisha kuwa afisa huyo sasa atajitenga hotelini kwa siku 14.

Mwandalizi Mkuu wa Michezo hiyo, Seiko Hashimoto, amesema hali hiyo imezua wasiwasi mkubwa, kwa wanamichezo wanaokuja kushiriki kwenye michezo hii.

Ripoti zinasema, afisa huyo alipowasili jijini Tokyo alipimwa na hakuwa na virusi hivyo lakini alipokwenda kwenye kijiji hicho cha wachezaji, alibainika kuwa na virusi hivyo.