JAPANI-HAKI

Japani: Wamarekani wawili wahukumiwa kifungo kwa kumsaidia Ghosn kutoroka

Mahakama ya Japan imewahukumu afisa wa zamani wa vikosi maalum vya Marekani na mtoto wake kwenda jela kwa kumsaidia kutoroka Carlos Ghosn.
Mahakama ya Japan imewahukumu afisa wa zamani wa vikosi maalum vya Marekani na mtoto wake kwenda jela kwa kumsaidia kutoroka Carlos Ghosn. - FAMILY HANDOUT/AFP/File

Mahakama ya mjini Tokyo, nchniJapan imemhukumu leo Jumatatu afisa wa zamani wa vikosi maalum vya Marekani na mtoto wake kwenda jela kwa kumsaidia kiongozi wa zamani wa kampuni ya magari Nissan, Carlos Ghosn, kutoroka Japan mwishoni mwa mwaka wa 2019, ambapo alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya ubadhirifu wa kifedha.

Matangazo ya kibiashara

Michael Taylor na mtoto wake Peter Taylor, ambao walikiri mashtaka mwezi uliopita kwa mashtaka dhidi yao walihukumiwa kwenda jela.

Michael Taylor alihukumiwa kifungo cha miezi 24 na mwanae miezi 20.

Carlos Ghosn, ambaye anakanusha mashtaka ya ubadhirifu wa kifedha dhidi yake, alitoroka Japan, ambako alikuwa nje kwa dhamana yenye masharti makali na kwenda Beirut, lakini haijaeleweka aliwazaje kukwepa ulinzi hadi kufika Lebanon.

Mamlaka nchini Lebanon zimeshasisitiza kuwa Ghosn ambaye ana uraia wa Ufaransa, Lebanon na Brazil aliingia nchi hiyo kihalali na kwamba nchi hiyo haina makubaliano ya kubadilishana watuhumiwa na Japan.