Kumi na mbili wafariki dunia baada ya mvua kubwa kunyesha China
Imechapishwa:
Mkoa wa kati wa China wa Henan umekumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, na mji mkuu wa Zhengzhou umeathiriwa vibaya baada ya mvua kubwa kunyesha tangu miaka 1,000 iliyopita.
Huko Zhengzhou, jiji lenye zaidi ya watu milioni 12 lililoko kwenye ukingo wa Mto Njano, watu 12 wamepoteza maisha kwenye njia ya reli iliyofunikwa kwa maji yaliyosababishwa na mvua. Kwa jumla, karibu watu 100,000 wamehamishwa katika jiji hilo.
Mamilioni ya watu huko Henan wanakabiliwa na hali ngumu tangu mwishoni mwa wiki iliyopita kufuatia mvua isiokuwa ya kawaida kunyesha na kusababisha mito kadhaa kujaa haraka maji kwenye bonde kubwa la Mto Njano.
Huduma nyingi za usafiri wa treni zimesitishwa katika mkoa huo, barabara kuu nyingi pia zimefungwa, na sfari za ndege zimecheleweshwa na zingine kufutwa.