Marekani, Japan, Korea Kusini waitahadharisha Korea Kaskazini

Wendy Sherman, afisa wa ngazi ya juu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani
Wendy Sherman, afisa wa ngazi ya juu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani © Internet

Marekani, Japan na Korea Kusini zimetuma ujumbe mzito kwa Korea Kaskazini kutokana na uratibu wa sera zao, amesema Wendy Sherman, afisa wa ngazi ya juu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amesema.

Matangazo ya kibiashara

"Uratibu huu wa karibu unatuma ujumbe muhimu sana kwa Korea Kaskazini, kuionysha kuwa tuko pamoja na tumeungana katika njia yetu ya sera hii," Wendy Sherman amesema baada ya kukutana na manaibu waziri wa mambo ya nje wa Japani na Korea Kusini.

Mazungumzo ya pande tatu yalifanyika Tokyo licha ya uhusiano mbaya kati ya Japan na Korea Kusini, uliotokana na pande hizo kushumiana baada ya Japani kuingilia kijeshi Korea kabla na wakati wa Vita vya pili vya Dunia.

Naibu Waziri wa Mambo ya nje wa Japani Takeo Mori amesema ushirikiano wa pande tatu na Marekani ni muhimu kwa utenguaji nyuklia wa Korea Kaskazini.

Korea Kaskazini imekataa wito wa Marekani kwa kuimarisha masuala ya diplomasia tangu rais wa Marekani Joe Biden achukue madaraka kutoka kwa Donald Trump.