MAREKANI-USHIRIKIANO

Afisa mwandamizi wa Marekani kuzuru China katikati mwa mvutano wa pande mbili

Wendy Sherman, msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, amepangwa kukutana na wanadiplomasia wawili wa juu zaidi wa China na wawakilishi wengine wa nchi hiyo huko Tianjin, mji ulio kusini mashariki mwa mji mkuu Beijing.
Wendy Sherman, msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, amepangwa kukutana na wanadiplomasia wawili wa juu zaidi wa China na wawakilishi wengine wa nchi hiyo huko Tianjin, mji ulio kusini mashariki mwa mji mkuu Beijing. BRENDAN SMIALOWSKI POOL/AFP/File

Naibu waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani , Wendy Sherman, atazuru China tarehe 25 na 26 Julai, wizara ya Mambo ya Nje imetangaza, wakati mataifa haya mawili yenye nguvu kiuchumi duniani yanaendelea kuwa na uhusiano mgumu.

Matangazo ya kibiashara

Wendy Sherman, msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, amepangwa kukutana na wanadiplomasia wawili wa juu zaidi wa China na wawakilishi wengine wa nchi hiyo huko Tianjin, mji ulio kusini mashariki mwa mji mkuu Beijing.

Ziara hii itafanyika mwishoni mwa ziara ya pili ya mwakilishi wa Marekani huko Asia chini ya kipindi cha miezi miwili. Anatarajia kwenda Japan, Korea Kusini na Mongolia.

Katika taarifa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilmesema kuwa mazungumzo yaliyopangwa kufanyika nchini China ni sehemu ya "juhudi zinazoendelea za Marekani kuwa na mazungumzo ya ukweli (...) ili kuendeleza masilahi na maadili ya Marekani na kusimamia kwa uwajibikaji uhusiano (wa pande mbili) ".

Ikiwa ziara ya Wendy Sherman nchini China ilitarajiwa na baadhi ya waangalizi, haikuwa kwenye mpango wa ziara yake ya Asia iliyotangazwa wiki iliyopita.

Biden kukutana na Jinping kurejesha uhusiano wa nchi zao

Mazungumzo hayo yanaweza kutumika kama msingi wa mazungumzo yaliyoimarishwa kati ya Washington na Beijing, au hata mkutano unaowezekana kati ya Marais Joe Biden na Xi Jinping mwishoni mwa mwaka - kando ya mkutano wa G20 uliopangwa mwishoni mwa mwezi Oktoba nchini Italia.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, aliyenukuliwa na Shirika la Habari la New China, amesema kuwa ziara hiyo ilipendekezwa na Marekani.