UTURUKI-USALAMA

Arobini na tano wakufa maji katika pwani ya Uturuki

Boti hiyo ilizama kilomita 259 kusini magharibi mwa mji wa Kas, kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Uturuki.
Boti hiyo ilizama kilomita 259 kusini magharibi mwa mji wa Kas, kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Uturuki. (Carte : RFI)

Boti lililokuwa limebeba wahamiaji 45 lilizama Alhamisi jioni wiki hii, ajaliiliyotokea katika pwani ya kusini mwa Uturuki, Wizara ya Ulinzi ya Uturuki imesema leo Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Meli mbili za Jeshi la Wanamaji la Uturuki na ndege zinafanya shughuli za utafutaji na uokoaji, Wizara ya Ulinzi imeongeza.

Boti hiyo ilizama kilomita 259 kusini magharibi mwa mji wa Kas, kulingana na wizara hiyo.

Meli kubwa mbili zimetumwa kufanya shughuli ya utafutaji katika eneo hilo na zinafanya kazi kwa uratibu na ndege ya kikosi cha wanamaji katika mazingira magumu kutokana na hali mbaya ya hewa na hali ya bahari.