INDIA-MAJANGA

Sitini na saba waangamia kufuatia mafuriko nchini India

"Shughuli za uokoaji zinaendelea katika maeneo tofauti ya Satara, Raigad na Ratnagiri. Kwa sababu ya mvua kubwa na mito iliyojaa, tunakabiliwa na uzito fulani wa kusafirisha vifaa vya kuokoa wathiriwa haraka," afisa mmoja, ambaye hakutakajina lake litajwe amesema.
"Shughuli za uokoaji zinaendelea katika maeneo tofauti ya Satara, Raigad na Ratnagiri. Kwa sababu ya mvua kubwa na mito iliyojaa, tunakabiliwa na uzito fulani wa kusafirisha vifaa vya kuokoa wathiriwa haraka," afisa mmoja, ambaye hakutakajina lake litajwe amesema. - INDIAN NAVY/AFP

Takriban watu 67 wamefariki dunia katika jimbo la Maharashtra magharibi mwa India kufuatia mvua kubwa iliyosababisha maporomoko ya udongo na mafuriko, mamlaka nchini India imesema leo Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Mito ya Maharashtra ilivunja kingo baada ya maji kuondolewa kwenye mabwawa yaliyokuwa yamejaa. Mvua imenyesha zaidi ya milimita 200 kwa muda wa saa 24 kwenye Pwani ya Magharibi, hadi milimita 594 katika maeneo mengine.

"Mvua kubwa isiyotarajiwa ilisababisha maporomoko ya udongo katika maeneo mengi na kusababisha mafuriko," amesema Uddhav Thackeray, kiongozi wa serikali ya Maharashtra.

"Mabwawa na mito yamefurika. Tunalazimika kufungulia maji kutoka kwenye mabwawa na, kwa sababu hiyo, tunahamisha watu wanaokaa karibu na kingo za mito kwenda sehemu salama."

Jeshi lashiriki katika shughuli ya utafutaji na uokoaji

Jeshi la Wanamaji la India na Jeshi wanasaidia shughuli za uokoaji katika wilaya za pwani, alisema

Watu wasiopungua 36 walifariki huko Taliye, kilomita 180 kusini mashariki mwa Mumbai, wakati maporomoko ya udongo yalisomba sehemu kubwa ya kijiji kimoja kidogo, amesema Vijay Wadettiwar, waziri wa jimbo hilo.

Angalau watu wanne wamekufa baada ya jengo kuporomoka Mumbai na wengine 27 katika visa vinne vya maporomoko ya udongo katika maeneo mengine ya Maharashtra, maafisa wakuu wa eneo hilo wamesema.

Maafisa wa idara ya dharura na jeshi wakabiliwa na ugumu katika kazi yao

"Shughuli za uokoaji zinaendelea katika maeneo tofauti ya Satara, Raigad na Ratnagiri. Kwa sababu ya mvua kubwa na mito iliyojaa, tunakabiliwa na uzito fulani wa kusafirisha vifaa vya kuokoa wathiriwa haraka," afisa mmoja, ambaye hakutakajina lake litajwe amesema.

Maelfu ya malori yalikuwa wamekwama kwenye barabara kuu inayounganisha miji ya Bombay na Bangalore kusini mwa nchi, na barabara imejaaa maji, afisa mwingine wa Maharashtra amesema.

Mamia ya vijiji na makumi ya miji katika maeneo yaliyoathirika ya Maharashtra hayana umeme na maji safi, ameongeza.