INDIA-MAJANGA

India: Mvua kubwa yasababisha vifo vingi India

Shughuli ya kutafuta watu waliokosekana baada ya kuporomoka kwa nyumba, India, Julai 18, 2021.
Shughuli ya kutafuta watu waliokosekana baada ya kuporomoka kwa nyumba, India, Julai 18, 2021. REUTERS - NIHARIKA KULKARNI

Watu wengi wamepoteza maisha baada ya mvua kubwa kunyesha Magharibi mwa India. Ripoti ya awali ya mamlaka za mitaa inaripoti waathirika zaidi ya 100.

Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa idara ya dharura wamekuwa wakitafuta katika matope na chini ya vifusi vya nyumba kujaribu kupata watu walio hai baada ya maporomoko ya udongo na mafuriko yaliyosababisha vifo vingi Magharibi mwa nchi.

Shughuli za dharura, zilizofanywa na jeshi la majini na jeshi la anga, bado zinaendelea, lakini zinafanywa katika mazingira magumu kwa sababu ya mafuriko na maporomoko ya udongo. Barabara kadhaa hazipiti kama barabara kuu kati ya miji ya Bombay na Goa.

Katika taarifa kwa waandishi wa habari serikali ya Mahasatara imesema kuwa mvua hio imesababisha maporomoko ya matope, mafuriko na kuporomoka kwa jengo. Kupitia mtandao wa twitter Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amesema amehuzunishwa na tukio hilo na kuahidi kuwa walioathirika watapewa usaidizi na serikali.