VIETNAM

Vietnam yarekodi visa vingi vya maambukizi ya Corona

Baada ya kufaulu kudhibiti virusi kwa sehemu kubwa ya janga hilo, Vietnam inakabiliwa na kuongezeka kwa idadi ya visa vya mambukizi ya vrusi vya Corona vinavyosbabishwa na COVID-19, mji mkuu wa kibiashara wa Ho Chi Minh na majimbo jirani yanakabiliwa na kesi nyingi mpya.
Baada ya kufaulu kudhibiti virusi kwa sehemu kubwa ya janga hilo, Vietnam inakabiliwa na kuongezeka kwa idadi ya visa vya mambukizi ya vrusi vya Corona vinavyosbabishwa na COVID-19, mji mkuu wa kibiashara wa Ho Chi Minh na majimbo jirani yanakabiliwa na kesi nyingi mpya. AP - Hau Dinh

Vietnam imetangaza rekodi mpya ya maambukizi ya COVID-19, na kesi mpya 7,968 za maambukizi kwa siku moja, zaidi ya theluthi mbili zimeripotiwa katika mji wa Ho Chi Minh.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na takwimu kutoka Wizara ya Afya, rekodi ya awali ya kesi za aambukizi kwa kila siku ilikuwa 7.307.

Baada ya kufaulu kudhibiti virusi kwa sehemu kubwa ya janga hilo, Vietnam inakabiliwa na kuongezeka kwa idadi ya visa vya mambukizi ya vrusi vya Corona vinavyosbabishwa na COVID-19, mji mkuu wa kibiashara wa Ho Chi Minh na majimbo jirani yanakabiliwa na kesi nyingi mpya.

Siku ya Ijumaa Wizara ya Afya ilitangaza kwamba itaongeza muda wa watu kutotembea katika mji huo hadi Agosti 1 na kwamba itaweka hatua kali za kizuizi katika mji mkuu, Hanoi, kuanzia Jumamosi hii.

Hatua hizi ni pamoja na kuzuia mikusanyiko ya watu zaidi ya watu wawili na kukatizwa kwa usafiri wa umma.

Vietnam hadi sasa imerekodi visa 90,934 vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo angalau 370.