CHINA

Mafuriko nchini China: Idadi halisi ya vifo Zhengzhou yazua mkanganyiko

Kwenye mlango wa barabara ya chini ya ardhi iliyokumbwa na mafuriko huko Zhengzhou, Julai 22, 2021
Kwenye mlango wa barabara ya chini ya ardhi iliyokumbwa na mafuriko huko Zhengzhou, Julai 22, 2021 AFP - NOEL CELIS

Nchini China, watu wasiopungua 58 wamefariki dunia na wengine 5 hawajulikani waliko mpaka sasa kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya mafuriko katika mkoa wa Henan, ambapo zaidi ya wakaazi milioni moja wamelazimika kuyahama makaazi yao. 

Matangazo ya kibiashara

Kumeibuka maswali juu ya idadi ya waathiriwa katika mji mkuu wa Zhengzhou, ambapo shughuli ya usafishaji wa barabara za chini ya ardhi zilizokuwa zimejaa maji.

Manispaa ya jiji la Zhengzhou haijatoa taarifa rasmi. Karibu magari 200 yamepatikana na madereva au abiria wanne walikufa maji baada ya kusombwa na maji, kulingana na afisa wa idara ya uokoaji akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina kwenye tovuti ya habari ya Pengpai. Vifo vinne kwa jumla ya magari 200: hii inatia mashaka makubwa. "Tutalazimika kufuatilia mahandaki," mwanasheria mmoja alisema.

Miongozo kwa vyombo vya habari

Kama ilivyo katika aina hii ya majanga, mamlaka inataka kuzuia picha za wahanga zisirushwe kwenye vyombo vya habari. Majanga ya asili ni tukio ambalo linatakiwa uangalizi mkubwa, ili kukabiliana na ukosoaji wa ukosefu wa maandalizi.

Maagizo yalitolewa kwa vyombo vya habari: "Toweni habari kuhusiana na shughuli za uokoaji, msichapishe habari au kurusha picha ambazo hazijaruhusiwa zinazoonyesha miili ya watu waliofariki kutokana na mafuriko haya. "Hii haikuzuia baadhi ya watumiaji wa mtandao Jumamosi hii kudai kwenye mitandao ya kijamii kwamba wapendwa wao walitoweka kwenye mahandaki au barabara za chini ya ardhi huko Zhengzhou.