AUSTRALIA

Australia kufidia baadhi ya ndugu wa "kizazi kilichoibiwa"

Waziri Mkuu wa Australiz Scott Morrison.
Waziri Mkuu wa Australiz Scott Morrison. William WEST AFP/File

Australia imetangaza Alhamisi kuwa itatoa fidia ya dola 75,000 za Australia (euro 46,853) kwa baadhi ya ndugu wa "kizazi kilichoibiwa".

Matangazo ya kibiashara

Neno "kizazi kilichoibiwa" linamaanisha sera ya uhamasishaji, inayobaini kwamba kuanza mwaka 1910 hadi 1970, watoto kutoka watu wa jamii asilia walichukuliwa kutoka kwa familia zao kwenda kulelewa katika familia za wazungu.

Ndugu wa watu hao watapokea dola 75,000 kwa uharibifu uliotokea wakati wa tukio hilo na nyongeza ya dola 7,000.

"Hii ni hatua ya muda mrefu ambayo inatambua uhusiano kati ya uponyaji, utu, afya na ustawi wa ndugu wa vizazi vilivyoibiwa, familia zao na jamii zao," amesema Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison katika Bunge Alhamisi.

Watu walio chini ya umri wa miaka 18 ambao walichukuliwa kutoka kwa familia zao wakati wakiishi katika Jimbo kuu la Australia na Wilaya ya Kaskazini kabla ya kupatikana kwa uhuru, na pia katika Jimbo la Jervis Bay karibu na New South Wales watapewa fidia hii.

Makundi ya watu wa jamii asilia wamekaribisha hatua hiyo ya serikali, lakini wameonya kuwa bado kuna kazi ya kufanywa.

Australia mwaka jana ilisema itapitia upya sera yake ya watu wa jamii asilia baada ya kutambua juhudi za miaka kumi kwa kuboresha viashiria kama vile kuishi na elimu kushindwa.