JAPAN

Japan kuongeza tena vizuizi dhidi ya Corona

Wapita njia wakivaa barakoa wakipita mbele ya bango la kibiashara kwa michezo ya Olimpki Tokyo 2020, Machi 16, 2020 Tokohama.
Wapita njia wakivaa barakoa wakipita mbele ya bango la kibiashara kwa michezo ya Olimpki Tokyo 2020, Machi 16, 2020 Tokohama. AFP

Japan inajiandaa kuongeza vizuizi katika kudhibiti virusi vya Corona katika wilaya nane mpya Alhamisi wiki hii. Visa vya maambukizi vinaenelea kuripotiwa nchini humo wakati Michezo ya Olimpiki ikiendelea huko Tokyo, mji mkuu wa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Visa vya maambukizi ya COVID-19 vimeongezeka kwa kasi nchini Japan, na kuzidi visa 14,000 nchini kote jana Jumatano.

"Idadi ya maambukizi mapya yimeongezeka kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea," Waziri wa Uchumi Yasutoshi Nishimura ameliambia jopo la wataalam ambao amewafikishia pendekezo hili la kuongeza vizuizi.

Wataalam wameidhinisha pendekezo hilo, lakini Yasutoshi Nishimura amesma katika mkutano na waandishi wa habari kwamba baadhi ya maafisa walionya kuwa hali ni mbaya ambapo kunahitaji kutangazwa hali ya hatari  nchini kote - hoja iliyoungwa mkono na kiongozi wa chama cha madaktari na auguzi nchini Japan.

Wilaya sita, ikiwa ni pamoja na ile ya Tokyo, mji kunakopigwa Michezo ya Olimpiki, tayari ziko katika hali ya hatari hadi Agosti 31.