KOREA KASKAZINI-USALAMA

Korea Kaskazini yajaribu kombora jipya la masafa marefu

Korea Kaskazini yafanya majaribio ya makombora ya masafa marefu.
Korea Kaskazini yafanya majaribio ya makombora ya masafa marefu. via REUTERS - KCNA

Korea Kaskazini imesema imefanikiwa katika jaribio lake la kurusha kombora mpya umbali wa kilomita 1,500, ambalo lina uwezo wa kupiga Japan, mwishoni mwa wiki.

Matangazo ya kibiashara

Korea Kaskazini imefanya jaribio hilo wakati maazimio yanakataza Pyongyang kuendelea na mipango yake ya silaha za nyuklia.

Hili ni jaribio la kwanza la urushaji wa kombora tangu mwezi Machi, shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini KCNA limesema Jumapili (Septemba 12). Jaribio hili linatishia usalama wa majirani zake, imesema Pentagon baada ya jaribio hilo. "Zoezi hili linaonesha kibbri cha Korea Kaskazini kuendeleza mpango wake wa nyuklia na vitisho ambavyo vinatia wasiwasi majirani zake na jamii ya kimataifa," imesema taarifa hiyo ya Pentagon.

Kwa kukiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa, majaribio yake ya hivi karibuni katika Bahari ya Japan yalitafsiriwa kama ishara ya kukaidi utawala wa rais wa Marekani Joe Biden, ambaye yuko madarakani tangu mwezi wa Januari mwaka huu. Majaribio mapya ya makombora ya Jumamosi na Jumapili yalihudhuriwa na maafisa wakuu wa Korea Kaskazini, kulingana na shirika hilo, ambalo linasema majaribio hayo yalifanikiwa