KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa Timu ya Taifa ya Argentina

Timu ya taifa ya Argentina
Timu ya taifa ya Argentina fifa.com

Timu ya taifa ya ArgetinaNi ya sita duniani, Imeshiriki kombe la dunia mara 15 na kunyakua taji hili mara 2 mwaka 1978 walipokuwa wenyeji na mwaka 1986 nchini Mexico.

Matangazo ya kibiashara

Wachezaji wa kuangaliwa

Lionell Messi ambaye aliwahi kushinda taji la mchezaji bora duniani miaka minne mfululizo tangu mwaka 2009 hadi 2012.

Wachezaji wengine ni pamoja na Carlos Tevez, Javier Mascherano na Angel Di Maria, wote ambao uzoefu katika ligi mbalimbali barani Ulaya.

Kocha mkuu

Alejandro Sabella

Mchezaji wa zamani wa Argetina na amekuwa kocha tangu mwaka 2011.

Wachezaji waliovuma

Daniel Passarella, Diego Maradona, Gabriel Batistuta, Mario Kempes