KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa Timu ya Taifa ya Honduras

Timu ya taifa ya Honduras
Timu ya taifa ya Honduras fifa.com

Timu ya taifa ya Honduras.Imeshiriki katika kombe la dunia mara 2 mara ya kwanza mwaka wa 1982 na 2010 nchini Afrika Kusini.Ni 32 duniani na haijawahi kushinda kombe la dunia.

Matangazo ya kibiashara

Wachezaji wa kuangaliwa

Emilio Izaguirre- Beki inayeichezea klabu ya soka ya Scotland ya Celtic na msimu wa mwaka 2010/2011 alitajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka.

Kipa na nahodha Noel Valladares pia ni mchezaji mwenye uzoefu na aliisaidia timu yake kufuzu katika kombe la dunia nchini Afrika Kusini mwaka 2010.

Wilson Palacios anayechezea klabu ya Stoke City ya Uingereza pia ni mchezaji wa kuangaliwa katika timu hii.

Wachezaji wengine ni pamoka na Carlo Costly na Jerry Bengtson wote ambao wana uzoefu mkubwa kucheza barani Ulaya.

Kocha mkuu

Luis Fernando Suarez raia wa Colombia, aliteuliwa kuwa kocha mwaka wa 2011 na amewahi pia kuwa kocha wa timu ya taifa ya Ecuador kati ya mwaka mwaka 2004 hadi 2007.

Wachezaji waliovuma

Amado Guevara, Carlos Pavon na Danny Turcios.