KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa Timu ya Taifa ya Iran

Timu ya taifa ya Iran
Timu ya taifa ya Iran fifa.com

Timu ya taifa ya IRANImeshiriki mara 3 mwaka 1978, 1998 na 2006 haijawahi kushinda taji lolote na ni ya 37 duniani.

Matangazo ya kibiashara

Wachezaji wa kuangaliwa

Nahodha Javd Nekounam ambaye anategemewa sana kutoa uongozi kwa wachezaji wenzake.

Masoud Shojaei mchezaji wa zamani wa klabu ya Osasuna, Reza Ghoochannejhad anayesalata soka la kulipwa nchini Ubelgiji na Ashkan Dejagah anayesakata soka katika klabu ya Fulham nchini Uingereza.

Kocha mkuu

Carlos Queiroz raia wa Ureno ambaye alianza kuifunza Iran mwaka 2011.

Aliwahi kuwa kocha wa Ureno kati ya mwaka 1991-1993, mwaka 2000-2002 akaifunza Afrika Kusini kabla ya kuifunza tena Ureno kati ya mwaka 2008-2010.

Wachezaji wa zamani waliovuma

Ali Daei, Khodadad Azizi, Karim Bagheri