KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa Timu ya Taifa ya Ufaransa

Timu ya taifa ya Ufaransa
Timu ya taifa ya Ufaransa fifa.com

Timu ya Taifa ya UfaransaLes Bleus imeshiriki katika kombe la dunia mara 13, na imeshinda mara moja tu mwaka 1998 walipokuwa wenyeji wa michuano hiyo na kuishinda Brazil kwa mabao 3 kwa 0 katika mchuano wa fainali.Ni ya 16 duniani kwa mujibu wa orodha ya Shirkisho la soka duniani.Mwaka 2006 ilifika fainali lakini ikaondolewa na Italia baada ya mikwaju ya penalti.Mwaka 2002 na 2010 Ufaransa iliondolewa katika hatua ya makundi.Ufaransa ilikuwa kati ya timu nne za kwanza kutoka barani Ulaya zilizoshiriki katika makala ya kwanza ya kombe la dunia yalipoanza mwaka 1930.

Matangazo ya kibiashara

Wachezaji wa kuangaliwa

Ufaransa inajivunia kuwa na wachezaji wenye uzoefu mkubwa wanaocheza soka katika ligi mbalimbali barani Ulaya, wakiwemo makipa Hugo Lloris na Steve Mandanda.

Wachezaji wengine ni pamoja na mabeki Eric Abidal, Laurent Koscielny na Raphael Varane.

Washambulizi, Franck Ribery, Karim Benzema na Olivier Giroud ambao licha ya kuwa na uwezo wa kufunga mabao wana uwezo mkubwa pia wa kumiliki soka uwanjani.

Kocha mkuu.

Didier Deschamps ambaye pia aliwahi kuwa kingo wa kati na mshambulizi wa timu ya taifa.

Kabla ya kuteuliwa mwaka 2012, aliwahi kuwa kocha wa klabu ya Monaco, Juventus na Marseille.

Wachezaji wanaokumbukwa

Just Fontaine, Michel Platini, Zinedine Zidane, Lilian Thuram, Thierry Henry, Patrick Viera, Laurent Blanc, Fabien Barthez, Didier Deschamps miongoni mwa wengine.