KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa Timu ya Taifa ya Uswis

Historia ya Switzerland Imefuzu katika kombe la dunia mara tisa mwaka (1934, 1938, 1950, 1954, 1962, 1966, 1994, 2006 na 2010) haijawahi kushinda taji lolote na ni ya nane katika orodha ya timu bora duniani.Imefika katika hatua ya robo fainali mara tatu, na mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 1954 walipokuwa wenyeji wa michuano hii.Mwaka 1994 na 2006 ilifika katika hatua ya makundi.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Uswis
Wachezaji wa timu ya taifa ya Uswis fifa.com
Matangazo ya kibiashara

Wachezaji wa kuangaliwa

Kipa Diego Benaglio,ni mmoja wa wachezaji wa kungaliwa katika michuano hii kutokana na usaidizi wa kuisadia klabu yake ya Wolfsburg ya Ujerumani mwaka 2009.

Wachezaji wengine ni pamoja na Tranquillo Barnetta, Gokhan Inler na Philippe Senderos pamoja na wachezaji chipukizi Xherdan Shaqiri, Fabian Schar, Granit Xhaka na Valentin Stocker.

Kocha mkuu

Kocha wa timu hii ni Ottmar Hitzfeld mchezaji wa zamani wa Ujerumani napia aliwahi kuwa kocha wa vlabu mbalimbali nchini humo kama Bayern Munich, Borrusia Dortmund kabla ya kuteuliwa kocha wa Switerland mwaka 2008.

Wachezaji maarufu waliostaafu

Alexander Frei, Stephane Chapuisat, Johann Vogel, Hakan Yakin