Wasifu wa timu ya taifa ya Ghana
Imechapishwa: Imehaririwa:
Timu ya taifa ya Ghana.Ni mwakilishi mwingine wa Afrika katika michuano hii.Imeshiriki mara 2, mwaka 2006 na 2010 haijawahi kushinda taji lolote na ni ya 38 duniani.Mwaka 2010 nchini Afrika Kusini ilifika katiak hatua ya robo fainali lakini ikaondolewa na Uruguay kupitia mikwajuju ya penalti baada ya mshmabulizi matata Asamoah Gyan kukosa penalti muhimu.Ghana ingekuwa timu ya kwanza kutoka barani Afrika kufuzu katika hatua ya nusu fainali.
Wachezaji wa kuangaliwa.
Viungo wa Kati wenye uzoefu mkubwa Michael Essien na Sulley Muntari.
Wengine ni pamojha na Andre Ayew, Kwadwo Asamoah na Kevin-Prince Boateng, bila kumsahau mshambulizi Asamoah Gyan.
Kocha mkuu.
Kwesi Appiah- Amekuwa kocha wa Blacks Stars tangu mwaka 2012 kabla ya hapo alikuwa kocha wa timu ya taifa chini ya umri wa miaka 23.
Wachezaji waliovuma
Abedi Pele, Samuel Kuffour, Ibrahim Sunday