KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa Timu ya Taifa ya Ujerumani

Kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani
Kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani fifa.com

Timu ya taifa ya UjerumaniImeshiriki mara 17, imeshinda mataji matatu mwaka 1954, 1974 na 1990 ya kombe la dunia ni ya pili duniani katika orodha ya FIFA.Ujwerumani imemaliza ya pili mara nne -1966, 1982, 1986 na 2002.Nafasi ya tatu mara mbili 1934 na 1970.Mwaka 2006 na 2010 walifika katika hatua ya fainali lakini hawakubahati kupata ushindi.

Matangazo ya kibiashara

Wachezaji wa kuangaliwa.

Kipa Manuel Neuer ambaye anafuata nyayo za wenzake Oliver Kahn na Jens Lehmann.

Wengine ni pamoja na Philipp Lahm, Bastian Schweinsteiger, Mesut Ozil, Thomas Muller, Marco Reus, Andre Schurrle, Toni Kroos na Mario Gotze.

Kocha mkuu

Joachim Low-Mchezaji wa zamani wa Ujerumani na amekuwa kocha tangu mwaka 2006.

Low pia alikuwa kocha msaidizi wa Ujerumani kati ya mwaka 2004 na 2006.

Wachezaji waliovuma

Franz Beckenbauer, Gerd Müller, Lothar Matthaus