CECAFA-MICHUANO 2014

Ethiopia yajiondoa katika maandalizi ya CECAFA

Wachezaji 12 wa timu ya Erythrea walliotoweka Kenya baada ya michuano ya CECAFA.
Wachezaji 12 wa timu ya Erythrea walliotoweka Kenya baada ya michuano ya CECAFA. AFP

Afrika Mashariki na Kati, mwaka huu michuano ya soka ya kila mwaka ya CECAFA, hayakufanyika kama ilivyopangwa baada ya wenyeji Ethiopia kujiondoa katika dakika za lala salama.

Matangazo ya kibiashara

Ethiopia iliratibiwa kuwa wenyeji wa michuano hiyo ya kila mwaka kuanzia tarehe 24 mwezi Novemba hadi tarehe 9 mwezi huu wa Desemba.

Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye alisema Ethiopia ilisema haingweza kuandaa michuani hiyo kwa sababu ya shughuli nyingi za kinyumbani na Kimataifa.

Awali, Musonye alikuwa amedokeza kuwa Sudan ingechukua nafasi hiyo lakini haikuwa hivyo.

Rwanda itakuwa mwenyeji wa michuano ya mwaka ujao wa 2015.