Soka Barani Afrika-AFCON 2015

Florent Ibenge: "DRC imeahidi kuibuka mshindi"

Wachezaji wa DRC wakisherehekea nafasi yao ya tatu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015.
Wachezaji wa DRC wakisherehekea nafasi yao ya tatu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO

Timu ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imenyakua medali ya shaba ya michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika Afcon 2015 kwa penalti (4-2) baada ya kutoka sare ya kutofungana Jumamosi Februari 7 dhidi ya Eqautorial Guinea katika uwanja wa Malabo.

Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa timu ya taifa ya Congo wanabaini kwamba walikua na matumaini ya kushinda mchuano huo dhidi ya Equatorial Guinea, licha ya kuwa kulikua na changamoto.

Nafasi hii ya tatu inapelekea timu ya taifa ya Congo kua na hatma nzuri, kwa mujibu wa kocha Florent Ibenge.

Florent Ibenge, kocha wa DRC:

" Hatukucheza mchezo mzuri zaidi. Timu yetu na Equatorial Guinea tumeghadhabishwa kuona hatuakufikia hatua ya fainali. Wakati mambo yanakwenda kama hivi, hali hiyo haiwezi kupelekea kuweko na mechi kubwa. Tulitaka mechi hii iwe na msisimko lakini haikua jinsi tulivyopanga. hata hivyo tulionesha mchezo mzuri katika mchuano huu, kama tulivyoahidi kuwa tutashinda mchezo huu. Tuna mradi wa kushinda michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika katika mwaka 2017 au 2019. Baadhi ya wachezaji watastaafu na tutasajili wengine. haya ndio mazingira tuanyoishi emo. "

Robert Kidiaba, mlinda lango wa DRC :

" Najisikia furaha kwa mchezo wangu wa mwisho kwa timu ya taifa. Sijui nini cha kusema, lakini itabidi nioneshe furaha yangu kwa Congo. [...] Mimi kwa kweli nilikuwa nmedhamiria katika mchuano huu wa mwisho, kwa sababu nilipokea simu nyingi kutoka Congo. [...] Nafasi hii ya tatu ni nzuri zaidi kuliko ushindi wa CHAN (2009). Hapa ni CAN! Ni bora kuliko ushindi katika michuano ya CHAN. "

Neeskens Kebano, kiungo wa kati wa DRC :

" Wakati unaangalia mchezo, unakuta kwamba wachezaji wa Equatorial Guinea walikua walijiandaa kimazoezi. mna hii ilipelekea timu hizi mbili kwenda sare ya kutofungana, lakini walikuja kushindwa wakati wa mikwaju ya penalti. [...] Ni sifa kubwa kwa kweli kwa DRC kufunga mechi hi. Equatorial Guinea ilitukabili na kutuweka katika wasiwasi mkubwa. Hata kushinda wangelishinda. Kaw hio ushindi huu unatupa medali. [...] Tunatarajia kwenda hata juu katika michuano ya Afcon ijayo. "

Jérémy Bokila, mshambuliaji wa DRC :

" Ilionekana tu kwamba wachezaji wa timu zote mbili walikuwa wamechoka, kwa sababu hapakuwa na fursa ya kuingiza bao. Sisi tulikuwa tulicheza Jumatano na Equatorial Guinea Alhamisi. Sote tuliku tumechoka. [...] Ni vizuri kuna tumepokea medali hii. Timu inatoka mbali. [...] Mchuano haukuwa rahisi na sisi tulikua katika hali ngumu. Lakini tunaweza kwenda nyumbanitukiwa na matumaini ya kufanya vizuri katika michuano kama hiyi miaka ijayo. "

Rui, beki wa Equatorial Guinea :

" Najisikia nimechoka kwa sababu tulicheza michuano miwili katika baada ya kupumzika kwa muda wa masaa 48. Tlijaribu kupambana ili tupate nafasi ya tatu, bila mafanikio. Baada ya mikwaju ya penalti kwa sababu ni bahati nasibu, tulijikuta tunakosa nafasi hiyo. Lakini nina furaha kwa timu yangu, kufuatia ilivyoonesha mchezo. Kwa sababu kwa muda mfupi, tulifanikiwa mambo makubwa. Kila mtu anajua ni vigumu kuunda timu katika siku 20. "

Ellong Doualla, kiungo wa kati wa Equatorial Guinea :

" Najisikia kutoridhika. Ningependa niondoke na medali. Lakini mimi nafurahia nafasi hii ya 4 tu ambayo ina maana kubwa kwangu na kwa wenzangu. "