LIBYA

Mashambulizi ya NATO yawasaidia Waasi kusonga mbele dhidi ya Vikosi vya Kanali Gaddafi

Malori yakikatiza katika Jiji la Misurata huku moto ukiendelea kuwaka baada ya kutokea kwa mashambulizi
Malori yakikatiza katika Jiji la Misurata huku moto ukiendelea kuwaka baada ya kutokea kwa mashambulizi © Reuters

Mashambulizi ya Majeshi ya Kujihami ya Nchi za Kujihami za Magharibi NATO nchini Libya yamefanikisha kuvirejesha nyuma vikosi vya Kiongozi wa taifa hilo Kanali Muammar Gaddafi katika Jiji la Misurata wakati Waasi wakisonga mbele.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo ya NATO yameutikisa pia Mji Mkuu Tripoli na hivyo kuwapa mwanya Waasi kuzidi kusonga mbele wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa UN umetoa onyo misaada ya kibinadamu inahitajika.

Tukio hilo la mashambulizi linakuja baada ya Katibu Mkuu wa NATO Andres Fogh Rasmussen na kusema muda wa utawala wa Kanali Gadafi kuondoka madarakani umewadia.

Waasi wamejigamba kuwa wamefanikiwa kuvirejesha nyuma vikosi vya Kanali Gaddafi katika eneo la Magharibi la Jiji la Misurata na sasa wanajiandaa kufanya mashambulizi zaidi.

Msemaji wa Waasi Ahmad Hassan amejigamba wamefanikiwa kusonga mbele Kusioni na Mashariki mwa Jiji la Misurata ambapo wamewaua wanajeshi wa kanali Gaddafi huku waasi wanane na wananchi kadhaa wakijeruhiwa.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya kushuhudia mapigano makali Waasi wanaendelea kupata utawala katika Jiji la Misurata ambalo ni la tatu kwa ukubwa ambalo limeshuhudia maelfu ya wakazi wake wakikimbia kupisha mapigano hayo.

Nazo takwimu zilizotolewa na Umoja wa Mataifa UN zimeonesha watu 750,00 wamekimbia nchini Libya tangua kuanza kwa mashambulizi yanayofanywa na Waasi katika taifa hilo.

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa UN anayeshughulikia Misaada ya Kibinadamu Valerie Amos amesema mapigano yanayoendelea yamekuwa chanzo cha kuharibika kwa mkundombinu na ukosefu wa fedha kwa wananchi wengi.

Valerie Amos - Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa UN Anayeshughulikia Misaada ya Kibinadamu

Amos ameongeza kuwa licha ya uwepo wa matatizo hayo lakini nchini ya Libya itageuka kuwa makaburi ya halaiki kutokana na wananchi wengi kuendelea kupoteza maisha kwenye ghasia zinazoendelea.

Nalo Shirika la Msalaba Mwekundu limepeleka meli iliyosheheni misaada ya kibinadamu lakini wanatarajia kuifikisha kwa njia ya helkopta kutokana na kuogopa mashambulizi ambayo yanaendelea.

Tatizo kubwa kwa sasa nchini Libya ni hatua ya wananchi wengi kulikimbia taifa hilo na kuomba hifadhi ya ukimbizi katika nchi za Ulaya huku wengi wao wakikimbilia Italia.