POLAND-UJERUMANI

Mahakama nchini Ujerumani kumuachia huru John Demjanjuk

John Demjanjuk mlinzi wa zamani wa Kambi ya Mauaji ya Sobibor
John Demjanjuk mlinzi wa zamani wa Kambi ya Mauaji ya Sobibor Reuters

Mahakama Nchini Ujerumani iliyomkuta na hatia ya makosa ya mauaji John Demjanjuk mzaliwa wa Ukraine inatarajia kumuachia baadaye alhamisi kutokana na kubaini hana uwezo wa kusafiri pamoja na halia yake kiafya kutetereka.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu unakuja baada ya mapema Alhamisi Mahakama hiyo kumhukumu kifungo cha miaka mitano jela Demjanjuk mwenye umri wa miaka 91 kwa kosa la mauaji ya watu wanaokadiriwa kufikia 30,000.

Demjanjuk anatajwa kutekeleza mauaji hayo ya wayahudi nchini Poland wakati wa Vita vya Pili vya Dunia ambapo wakati huo alikuwa mlinzi katika Kambi ya Mauaji ya Sobibor.

Msemaji wa Mahakama hiyo Margarete Noetzel amesema sababu nyingine ambayo imewasukumua kuchukua uamuzi wa kumuachia huru Demjanjuk ni kutokana na kuwa na upofu wa macho hivyo hawezi kuleta madhara yoyote kwa umma.

Mzaliwa huyo wa Ukraine alipelekwa nchini Ujerumani mwaka 2009 akitokea Marekani hana uwezo wa kusafiri kutokana na kutokuwa na urai kwani mwaka 2002 alinyang'anywa uraia wa Marekani kutokana na kudanganya juu ushiriki wake kwenye vita.

Mtoto wake John Demjanjuk Jr alisema baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo familia yake ina mpango wa kukata rufaa juu ya adhabu ya kifungo cha miaka mitano ambayo amepewa baba yake.

Nao mawakili wa Demjanjuk walitofautiana na hukumu hiyo dhidi ya mteja wao na kuahidi kufanya mchakato wa kukataa rufaa kupinga uamuzi wa kutokana na hali ya afya ya mteja wao kuwa si ya kurudhisha.