LIBYA

Mkuu wa sera za mambo ya nje wa umoja wa ulaya Catherine Ashton awasili Benghazi

Catherine Ashton, mkuu sera za nje - Umoja wa Ulaya
Catherine Ashton, mkuu sera za nje - Umoja wa Ulaya Reuters

Mkuu wa sera za mambo ya nchi za nje wa umoja wa Ulaya EU, Catherine Ashton hatimaye amewasili nchini Libya katika ngome ya waasi wa nchi hiyo iliyoko katika mji wa Benghazi.

Matangazo ya kibiashara

Mara baada ya kuwasili katika mji wa Benghazi kiongozi huyo atakutana na viongozi wa tume ya taifa ya mpito ya nchi hiyo inayoongozwa na Mustafa Abdul Jalil na kufanaya mazungumzo kabla ya kuzindua rasmi ofisi za umoja wa Ulaya katika mji huo.

Akizungumzia ziara yake katika mji wa Benghazi, mkuu huyo wa sera za mambo ya nje wa umoja huo amesema kuwa inalenga kuzungumza na viongozi mbalimbali katika mji huo kama umoja huo ulivyoahidi kuwasaidia waasi hao.

Ameongeza kuwa ziara hiyo pia inalenga kukagua maeneo maalumu ambayo yatajengwa shule mpya pamoja na hospitali, huku pia akitangaza ukarabati mkubwa wa majengo ya shule na hospitali yaliyoharibiwa kukarabatiwa na umoja huo.

Ofisi za umoja wa ulaya zinatarajiwa kufunguliwa hii leo katika hoteli ya Benghazi.