Syria-EU

EU yamwekea vikwazo rais wa Syria

Bashar Al-Assad rais wa Syria aliyewekewa vikwazo na EU
Bashar Al-Assad rais wa Syria aliyewekewa vikwazo na EU REUTERS/Zohra Bensemra

Umoja wa ulaya, EU unatarajiwa kumwekea vikwazo rais wa SYRIA, Bashar al-Assad kwa mara ya kwanza ili kumshinikiza amalize utawala wake kwa njia za kidiplomasia na kuleta mabadiliko.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imefikiwa na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za umoja wa Ulaya katika mkutano wao mjini Brussels nchini Ubelgiji na wametangaza hatua watakazochukua dhidi ya Bashar Al Asssad na viongozi wengine.

Hatua zilizochukuliwa ni pamoja kufungiwa safari za nje na kutaifishwa kwa mali za Assad na mawaziri waliotajwa katika orodha ya watakaoathirika na vikwazo hivyo.

EU tayari imeshawawekea vikwazo ndugu wa karibu wa Rais Bashar Al Assad na katika maandamano yaliyofanyika mwishoni mwa juma watu wapatao 44 wanadaiwa kuuawa ingawaje Serikali ilitangaza vifo vya watu 17.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wameeleza kuwa hatua zilizochukuliwa na EU zitasaidia kuweka msukumo katika kuleta madaliko ya kisiasa nchini Syria.