Pakistani-Taliban

Wapiganaji wa Taliban wavamia kituo cha kijeshi, waua watano

Wanajeshi wa Taliban wakiwa katika harakati za mashambulizi
Wanajeshi wa Taliban wakiwa katika harakati za mashambulizi Reuters

Wapiganaji wa kundi la Taliban, wakiwa na roketi na milipuo wamekivamia kituo kikuu cha jeshi la wanamaji katika jiji kubwa nchini Pakistan, na kuziharibu ndege mbili za doria na kuua watu watano.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa maelezo ya maofisa usalama jijini Karachi, shambulio hilo limetokea majuma matatu baada ya kuuwawa kwa Osama bin Laden na lilidumu kwa saa nane, tangu lilipoanza usiku wa manane.

Kufuatia tukio hilo, takriban wapiganaji kumi na watano wa Taliban, walijificha usiku wa kuamkia leo, wakitekeleza azma yao, ya kulipiza kisasi cha kuuawa kwa kiongozi wa mtandao wa Al Qaeda, duniani Osama Bin Laden.

Waziri wa mambo ya ndani wa Pakistani Rehman Malik amesema magaidi hao, waliingia kwa siri kituoni hapo kwenye jiji hilo lenye wakazi milioni 16, eneo ambalo majeshi ya NATO, hutunza misaada yake kwa nchi ya Afghanistan na kuanza mashambulizi.