Libya, Marekani, AU

Mapambano nchini Libya yashika kasi wakati rais Zuma akitaraji kuzuru Tripoli

REUTERS/Louafi Larbi

Majeshi ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO yameendelea na mashambulizi yao katika Jiji la Tripoli nchini Libya ikiwa ni njia mojawapo ya kuudhoofisha utawala wa Kanali Muammar Gaddafi.

Matangazo ya kibiashara

Wakati mashambulizi ya NATO yanazidi kushika kasi Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma anatarajiwa kuzuru Libya kukutana na Kanali Gaddafi kujadili mustakali wa utawala wake huku duru zikidokeza huenda akawa na lengo la kumtaka aondoke madarakani.

Barack Obama
OBAMA BARRACK KUHUSU LIBYA

Kwa upande wao Marekani na Uingereza wamezidi kujiapiza kupambana na Utawala wa Kanali Gaddafi huku Rais Barack Obama akiweka bayana nchi yake itaendelea kuwa mstari wa mbele kuwalinda wananchi.

Naye Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron hakusita kutia neno pale alipoamua kuunga mkono hatua ya nchi hiyo na mshirika wake Marekani kuendelea kuwalinda wananchi wa Libya.

Hali ya mambo nchini Libya imeendelea kuwa tete kipindi hiki ambacho Waasi wanaendelea kusaka uungwaji mkono na wakisaidiwa kusonga mbele kutokana na kutekelezwa kwa mashmbulizi ya NATO.