NIGERIA

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameapishwa hii leo na kuahidi makubwa wananchi wake

Goodluck Jonathan rais wa Nigeria
Goodluck Jonathan rais wa Nigeria AFP / PIUS UTOMI EKPEI

Hatimaye rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameapishwa rasmi hii leo mjini Abuja kuwa rais mpya wa taifa hilo katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Matangazo ya kibiashara

Hafla ya kuapishwa kwa kiongozi huyo zimefanyika chini ya ulinzi mkali mjini Abuja na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka barani afrika, huku rais Jonathan mwenyewe mwenye umri wa miaka 53 hivi sasa akiahidi kuwatumikia kwa moyo wananchi wa taifa hilo.

Rais jonathan alimshinda mpinzani wake jenerali wa zamani wa nchi hiyo Muhammadu Buhari katika uchaguzi wa mwezi april, uchaguzi ambao waangalizi wa jumuiya ya kimataifa walisema kuwa ulikuwa huru na haki.

Hata hivyo kushinda kwa kiongozi huyo kutoka aneo la kusini ambalo lina wakristo wengi kulisababisha machafuko kaskazini mwa nchi hiyo kwenye ngome ya mpinzani wake Buhari, na kusababisha watu zaidi ya 400 kupoteza maisha kutoka na vurugu hizo.

Rais Goodluck Jonathan aliongoza taifa hilo kwa muda baada ya kutokea kwa kifo cha rais Umaru Yar Adua mwaka jana, na sasa ataongoza taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani afrika kama rais rasmi.