UJERUMANI-ULAYA

Mawaziri wa kilimo wa Ulaya wanakutana kujadili hatma ya bakteria E.coli

Baadhi ya matunda ambayo bakteria wa E.coli wanasemekana kutokea
Baadhi ya matunda ambayo bakteria wa E.coli wanasemekana kutokea REUTERS/Fabian Bimmer

Mawaziri wa kilimo kutoka umoja wa Ulaya EU,wanafanya kikao cha dharura mjini Luxembourg Ujerumani,kujaribu kubaini chanzo na kutafuta suluhu kuhusu bakteria wa E.Coli ambao wamesababisha watu 22 kufariki dunia barani Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Vipimo vya awali vya kubaini chimbuko la baktreia hao,vilifanywa jana nchini Ujerumani na matokeo kuonyesha kutokuwepo kwa bakteria hao.

Kati ya vipimo 40 ambavyo vimefanywa Kusini mwa mji wa Hamburg,hadi sasa vipimo 23 vimethibitiswa kutoathiriwa na bakteria.

Zaidi ya watu elfu mbili hadi sasa kutoka mataifa12 barani ulaya wameathiriwa na maradhi hayo ya E.Coli,huku visa vyingi vikiripotiwa kwa wasafiri ambao wamekuwa ziarani nchini Ujerumani.

Serikali ya Ujerumani imekuwa ikiilaumu Hispani kuwa,bakteria hao ndiko walikotokea na kusambaaa hadi Ujerumani kutokana na kusafirishwa kwa matango nchini humo.

Tuhuma hizo zimepingwa vikali na serikali ya Hispania ambayo inataka Ujerumani kuifidia kwa asilimia mia moja kwa kile,Hispani inasema tuhma hizo zimesabisha taifa hilo kukosa soko la mboga na matunda na hivyo kupata hasara kuwbwa.

Mawaziri hao wanapokuwata,wanataka kujua kutoka kwa wataalam na wanasanyasi kiini cha bakteria hiyo,na chimbuko lake.