Syria

Majeshi ya Syria yaendeleza hujuma, huku hali ya kibinadamu ikiripotiwa kuwa mbaya

Waandamanaji wakimtaka rais wa Syria kusitisha mauaji dhidi ya raia
Waandamanaji wakimtaka rais wa Syria kusitisha mauaji dhidi ya raia REUTERS/Andrew Winning

Majeshi nchini Syria yanaendelea na operesheni ya kuwasaka waliotekeleza mauji ya wanajeshi zaidi ya mia moja Kaskazini mwa taifa hilo katika eneo la Jisr al-Shughur ,huku maelfu ya raia wakiendelea kukimbia nchi hiyo na kwenda kutafuta hifadhi nchini Uturuki.

Matangazo ya kibiashara

Majeshi hayo yamekuwa yakichoma moto nyumba za watu na kuteketeza mazao katika vijiji mbalimbali kasakazini mwa taifa hilo, katika operesheni inayoelezwa ni ya kulipiza kisasi dhidi ya mauji hayo ya wanajeshi.

Majeshi hayo yanatumia silaha hatari na helikopta katika operesheni hiyo, wanaoifanya kwa kujificha misituni na milimani.

Serikali ya Damas inataka kufifiza vuguvugu la maadamano ambalo kama inavyo sema serikali hiyo limechukuwa mkondo mwingine wa kuazisha uasi.

Hata hivyo operesheni hiyo imesababisha mtafaruku jeshini. Kulingana na mkimbizi alieutoroka mji wa Jisr al-Shughur, vifaru 4 viligeukana na kuanza kushambuliana na hivo kuthibitisha habari ya mtafaruku jeshini.

Mji huo wa Jisr al-Shughur  wenye wakaazi zaidi ya elfu 50, ulishuhudia mapambano makali wiki iliopita na kusababisha vifo vya askari polisi 120. serikali ya Bashar el Assad inayatuhumu makundi ambayo yameanza uasi. Lakini wapinzani na mashahidi wanasema ni mtafaruku ulioibuka jeshini uliosababisha askari hao kushambuliana.

Kulingana na asasi zisizokuwa za kiserikali, wapinzani 1.200 wameyapoteza maisha tangu Machi 15, huku wengine elfu 10 wakitiwa mbaroni.

kufuatia matukio hayo, wanamemba 4 wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa(Ufaransa, Uingereza, Ujerumani na Portugal) wamewasilisha azimio la kulaani mauaji hayo na kuyachukulia kama "Ukatili dhidi ya Binadamu" Azimio hilo latarajiwa kupigiwa kura Jumanne Juni 14. Rusia na China zinapinga yaliomo katika azimio hilo