Mazumgumzo ya kusaka amani Abyei yaendela huko Addis Ababa

Nyumba zilizo teketezwa kwa moto huko Abyei Mei 23
Nyumba zilizo teketezwa kwa moto huko Abyei Mei 23 Reuters

Mazungumzo ya kusaka muafaka wa mpaka, katika maeneo yaliyochangia kuzuka kwa machafuko nchini Sudan ya Abyei na Kordofan Kusini yameendelea leo bila hata hivyo kuwa na matumaini ya kupatikana makubaliano

Matangazo ya kibiashara

Tayari Rais Omar Hassan Al -Bashir, ameshaondoka jijini Adis Ababa, Ethiopia, na kuacha ujumbe wake huku viongozi wanaosimamia mjadala huo, wakisema kwa ujumla maafikiano yameanza kuonekana na wanaimani machafuko yatafikia kikomo.

Awali rais Al Bashir  ameripotiwa kusema mbele ya kiongozi wa kusini Salva Kiir katika mazungumzo ya Umoja wa Afrika yanayoendelea nchini Ethiopia kwamba yuko tayari kuyaondowa majeshi yake katika eneo la Abyei.

Sudan kusini inatarajia kujitenga na kaskazini katika mpango wa amani ambao ulimaliza miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya kusini na kaskazini, vilivyosababisha vifo vya watu takriban milioni moja na nusu.

Kuna wasiwasi kuwa mapigano ya hivi karibuni huenda yakazusha upya mgogoro huo, ingawa Rais Bashir amesema atakubaliana na uhuru wa kusini.

Waziri wa habari wa Sudan Kusini Barnaba Marial Benjamin amesema taarifa ya nini kitatokea iwapo majeshi ya kaskazini yataondoka bado zinafanyiwa kazi.

Sudan Kaskazini inalaumiwa kutokana na kupeleka majeshi yake huko Abyei, huku wachambuzi wa siasa wakitilia shaka kumalizwa kwa machafuko hayo, iwapo viongozi wenyewe hawatakuwa tayari.