Pakistani

Watu 5 wakamatwa nchini Pakistan baada ya kushukiwa kusaidia kuawa kwa Osama Bin laden

Ramani ya Pakistan
Ramani ya Pakistan DR

Shirika la ujasusi nchini Pakistan, ISI limewakamata watu watano ambao walilisaidia Shirika la Ujasusi la Marekani, CIA, kabla ya kumvamia na baadae kumuua kiongozi wa mtandao wa kigaidi duniani Osama bin Laden mwanzoni mwa mwezi Mei nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya jeshi kukana taarifa hizo, meja mmoja wa jeshi la Pakistan, anaripotiwa kunakili namba za magari yaliyokuwa yakiingia katika makazi ya Osama, huko Abbottabad, mji wa kijeshi ulio karibu na jiji la Islamabad.

Uhusiano wa kidiplomasia baina ya Pakistan na Marekani umeingia doa, kufuatia kuuwawa kwa Osama Bin Laden kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa Alqaida Mei 2 iliopita.

Pakistani inaishumutumu Marekani kuendesha operesheni ya aina hiyo katika ardhi yake bila hata hivyo kuitaarifu, huku Marekani ikisema ingelitowa taarifa kabla ya kutekekeleza operesheni hiyo isingelifaulu