LIBYA-GADDAFI

Kanali Gaddafi asisitiza nchi yake kuvishinda vikosi vya NATO na waasi

Kiongozi wa Libya, Kanali Muamer Gaddafi
Kiongozi wa Libya, Kanali Muamer Gaddafi REUTERS/FIDE Press service

Licha yakuendelea kwa mashambulizi makubwa katika mji wa tripoli nchini Libya na yanayofanywa na vikosi vya NATO kiongozi wa taifa hilo kanali Muamer Gaddafi ameendelea kusisitiza kuwa nchi yake itayashinda majeshi hayo.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya ijumaa kanali Gaddafi kupitia kituo cha televisheni alisikika akiongea kwa njia ya simu akishutumu vikali mashambulizi ya NATO katika mji wa Tripoli na kuahidi kuwa vikosi vyake vitaendelea kupambana na waasi hadi pale watakaposhindwa.

Kauli hiyo ya kanali inakuja wakati ambapo usiku wa kuamkia hii leo vikosi vya serikali vimeendelea na mashambulizi dhidi ya ngome za waasi katika mji wa Misrata ambako waasi wanaonekana kuzidiwa nguvu.

Kiongozi huyo amesema kuwa nchi yake haina mpango wa kubadili chochote kwa shinikizo toka jumuiya ya kimataifa, bali mabadiliko yatafanyika kwa maamuzi ya wananchi wa Libya na sio vinginevyo.

Kauli ya Gaddafi inaendelea kudhibitisha uimara wa vikosi vyake na yeye mwenyewe kutokuwa tayari kung'atuka madarakani wakati huu ambapo vikosi vya majeshi ya NATO yamezidisha mashambulizi katika mji wa Tripoli kwa kuahsmbulia makazi yake.

Siku ya alhamisi mtoto wa kiongozi huyo Seif al-Islam alitangaza kuwa baba yeke yupo tarai kuitisha uchaguzi mkuu nchini humo utakaopelekea kupatikana kwa serikali mpya ambayo itachaguliwa kidemokrasia bila kutumia mabavu.

Waasi wa Libya wamekuwa wakivilalamikia vikosi vya NATO kwa kushindwa kuwakabili wanajeshi wa serikali ambao wamekuwa wakiendesha operesheni za ardhini katika mji wa Misrat na miji mingine kwa lengo la kuwasambaratisha waasi hao.