Yemen-Alqaeda

Wapiganaji 13 wa Al Qaeda na wanajeshi 2 wauawa nchini Yemen

Wapiganaji nchini Yemen
Wapiganaji nchini Yemen AFP

Wapiganaji kumi na watatu, wanaosadikiwa kutoka katika mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda, wameuwawa hapo jana wakati wakikabiliana na majeshi ya serikali, ambapo askari wawili nao walipoteza maisha katika tukio hilo.

Matangazo ya kibiashara

Vyanzo vya kijeshi na kidaktari nchini Yemen, vimethibitisha juu ya vifo hivyo, vilivyotokea jijini Zinjibar, wakati askari hao wakijaribu kupambana na magaidi hao, kutoka Ansar al Sharia, waliokuwa wakitega mabomu katika barabara kuu.

Na wapinzani wa Rais Ali Abdullah Saleh, wanaishutumu serikali yake kwa kukuza machafuko hayo ya kidini, kwa lengo la kuupa dhamana, utawala wake wa miaka thelathini na mitatu.