FRANCE-WASHINGTON

Christine Lagarde asikilizwa alhamisi Juni 23 na bodi ya uongozi wa IMF

Christine Lagarde waziri wa uchumi wa Ufaransa anaewania uongozi wa IMF
Christine Lagarde waziri wa uchumi wa Ufaransa anaewania uongozi wa IMF Reuters

Waziri wa Uchumi wa Ufaransa Christine Lagarde, mgombea kwenye uadhifa wa ukurugenzi Ukuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF), anatarajiwa kusikilizwa Alhamisi Juni 23, 2011 na bodi ya taasisi hiyo kubwa.

Matangazo ya kibiashara

Mbali na ushindani kutoka Mexico na Agustín Carstens, pia mgombea huyo anakabiliwa na uchunguzi mpya katika mgogoro kati ya Club Lionnais na Bernard Tapie.

Christine Lagarde atasikilizwa Alhamisi Juni 23 na bodi ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) mjini Washington. Mgombea kwenye uadhifa huo uliachwa wazi na Dominique Strauss-Kahn aliejiuzulu baada ya kukabiliwa na tuhuma za ubakaji. Waziri huyo wa uchumi wa Ufaransa Christine Lagarde, atatakiwa kutowa maoni yake juu ya masuala yanayo likabili fuko hilo la fedha duniani na nchi wanachama wake. Atatakiwa pia kujibu maswala yote atayo ulizwa na bodi ya uongozi wa fuko hilo la IMF.

Christine Lagarde anashindana na Agustín Carstens ambae upande wake alisikilizwa Jumanne Juni 21 na Wanachama ishirini na nne. Wanachama hao watatakiwa kupata muafaka kati ya wagombea hao wawili. Ikiwa muafaka utakosekana watatakiwa kupigas kura na kumtangaza mshindi Juni 30