Uingereza-Marekani

Serikali ya Uingereza yatangaza kuanzisha mazungumzo na Taliban huko Afghanistani

William Hague
William Hague RFI

Serikali ya Uingereza imetangaza kuwa kwenye mazungumzo na Wanamgambo wa Taliban ambao maskani yao ni nchini Afghanistan wakisema hiyo itakuwa njia muafaka ya kumaliza hofu ya kiuslama iliyojitokeza. 

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza William Hague amethibitisha kuanza kwa mazungumzo hayo ambayo yamekuja baada ya yeye kufanya ziara nchini Afghanistan kuangalia namna ya kurejesha amani.

Waziri Hague amesema huu ni wakati muafaka wa kuwa na mchakato wa kisiasa katika kuhakikisha kila ambacho kipangwa kwa ajili ya kuimarisha usalama wa Afghanistan baada ya muda wao kukamilika kinafanikiwa.