Japani

Tetemeko la ardhi laikumba Japani kwa mara nyingine tena

Kituo cha Nyukilia cha Fukushima kilicho haribiwa na tetemeko la ardhi cha Futaba,Machi 12,2011.
Kituo cha Nyukilia cha Fukushima kilicho haribiwa na tetemeko la ardhi cha Futaba,Machi 12,2011. Jiji Press / AFP

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa richa sita nukta saba limeikumba nchi ya Japan hii leo, na mamlaka husika kutoa onyo, huenda ikatokea sunami nyingine.

Matangazo ya kibiashara

Wakazi wa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, kilomita hamsini ng'ambo ya kisiwa cha Mikayo, katika bahari ya Pasific, wameamshwa kwa tetemeko hilo, lililosababisha mshtuko mkubwa, na kuwakumbusha janga la tarehe 11 mwezi Machi.

Hatahivyo wakala wa hali ya hewa wameondoa onyo hilo, saa moja baada ya kutokea tetemeko hilo, lililofikia kina cha kilomita 32 chini ya ardhi.

Na viongozi wa serikali za mitaa, wameamuru raia katika nyumba zisizopungua elfu nane kuyahama makazi yao, huko Iwate ili kuepuka athari zinazoweza kutokea.