Ufaransa

Kesi ya aliekuwa mkurugnezi mkuu wa IMF yachukuwa sura mpya

Sakata la ubakaji linalomwandama mkurugenzi mkuu wa zamani wa shirika la fedha duniani IMF Dominique Straus Kahn linazidi kuchukua sura mpya, na hivi leo mwanamke mwingine raia wa Ufaransa amejitokeza na kusema kuwa atamfugulia mashtaka ya ubakaji Strauss Khan.     

e Dominique Strauss-Kahn na mkewe Anne Sinclair wakiwasili mahakamani Manhatan Julay mosi 2011.
e Dominique Strauss-Kahn na mkewe Anne Sinclair wakiwasili mahakamani Manhatan Julay mosi 2011. reuters/M.Segar
Matangazo ya kibiashara

Tristane Banon mwanahabari na mwandishii wa vitabu kupitia kwa wakili wake, anasema kuwa Strauss-Kahn alimbaka wakati alipokuwa anamhoji mwaka wa 2002 mjini Paris Ufaransa.
 

Wakati hayo yakijiri Sakata la kesi ya mkuu huyo zamani wa shirika la fedha duniani, Dominique Strauss Kahn limeingia katika mkondo mwingine baada ya jopo la watetezi wa Kahn kukanusha madai ya jarida moja la mjini New York kuwa Kahn alijihusisha na vitendo vya Ngono na mhudumu wa Hoteli kama njia ya kupata pesa.

jarida hilo hapo jana liliripoti kuwa Mshtaki huyo alifanya ngono na kahn akitarajia kupata pesa yake baada ya tendo hilo,lakini kahn akakaidi na kuongeza kuwa mhudumu huyo hufanya ngono na wanaume wageni hotelini ili kujipatia pesa.

jopo hilo likiongozwa na mwanasheria Benjamin Brafman na William Taylor,limesema hakukuwa na makubaliano ya namna hiyo kati ya pande hizo mbili.

Wakati tuhuma dhidi ya Kahn zikiendelea ,kesi nayo inakaribia kufikia ukingoni baada ya waendesha mashtaka kugundua kuwa mhudumu huyo alidanganya kuhusu kesi hiyo,huku akihusishwa na vitendo vya uhalifu kama biashara ya dawa za kulevya na kujipatia fedha isivyo halali.