TRIPOLI - MOSCOU

Serikali ya Libya ya kanusha kuwepo na majadiliano kuhusu kuondoka kwa Gaddafi.

AFP

Habari kuhusu kuwepo kwa majadiliano juu ya kuacha madaraka kwa Kanali Muamar Gaddafi na kubaki katika mahali salama nje aidhaa ndani ya libya zimekanushwa na msemaji wa serikali ya Libya Moussa Ibrahim.

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo yaliopo ni kuhusu kusitisha mtuto, jinsi ya kuagiza misaada ya kibinadamu, na kuanzisha mazungumzo kati ya raia wa libya. Hatuwa ya nne itakuwa ni ya utawala wa mpito utaobadili mfumo wa siasa ya nchi hiyo ambapo wananchi ndio wataokuwa wakiamuwa hatma ya viongozi.

“Hakuna lolote lakujadili kuhusu Gaddafi, huo ndio msimamo wetu wa kimsingi. Hatma ya Libya inatakiwa kujadiliwa na wa libya wenyewe. Gaddafi ni ishara ya utamaduni wa kihistoria, wa Libya wako tayari kufa juu ya kumlinda”

Gazeti la Urusi la Kommersant toleo la jumanne hii lilichapisha habari kwamba Gaddafi yuko tayari kuacha madaraka iwapo atahakikishiwa usalama.

Gaddafi yuko tayari kuondoka madarakani lakini anataka ahakikishiwe usalama, limeandika Gazeti la Kommersant na kutaja chanzo cha juu kutoka serikali ya Urusi.

Chanzo hicho kinasema kwamba nchi kadhaa zipo tayari kumpokea Gaddafi ikiwemo Ufaransa.

Toleo la habari hiyo kwenye Gazeti hilo limeongeza kuwa Gaddafi angependa mwanae Saif al Islam awanie urais iwapo ataondoka madarakani.